Job 36

Elihu Atukuza Wema Wa Mungu

1Elihu akaendelea kusema:
2 “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha
kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.

3 aNinayapata maarifa yangu kutoka mbali,
nami nitamhesabia haki Muumba wangu.

4 bUwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo;
mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.


5 c“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu;
ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.

6 dHawaachi waovu waendelee kuishi,
bali huwapa walioteswa haki yao.

7 eYeye haondoi macho yake kwa wenye haki;
huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme
na kuwatukuza milele.

8 fLakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo,
wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,

9 ghuwaonyesha yale waliyoyatenda,
kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.

10 hHuwafanya wao kusikia maonyo,
na huwaagiza kutubu uovu wao.

11 iKama wakitii na kumtumikia,
wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio,
na miaka yao katika utoshelevu.

12 jLakini wasiposikiliza,
wataangamia kwa upanga,
nao watakufa pasipo maarifa.


13 k“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki;
hata anapowafunga, hawamwombi msaada.

14 lWanakufa wangali vijana,
miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

15 mBali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao,
na kuzungumza nao katika dhiki zao.


16 n“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki,
ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi,
hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.

17 oLakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu;
hukumu na haki vimekukamata.

18 pUwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri;
usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.

19 qJe, utajiri wako hata nguvu zako nyingi
vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?

20 rUsiutamani usiku uje,
ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.

21 sJihadhari usigeukie uovu,
ambao unaupenda zaidi kuliko mateso.


22 t“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake.
Ni nani aliye mwalimu kama yeye?

23 uNi nani aliyemwelekeza katika njia zake,
au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?

24 vKumbuka kuzitukuza kazi zake,
ambazo watu wamezisifu katika wimbo.

25 wWanadamu wote wameiona;
watu wanaikazia macho kwa mbali.

26 xTazama jinsi Mungu alivyo mkuu,
kupita ufahamu wetu!
Hesabu ya miaka yake haitafutiki.


27 y“Yeye huvuta juu matone ya maji,
ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;

28 zmawingu huangusha chini maji yake,
nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.

29 aaNi nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu,
jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.

30 abTazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka,
naye huvifunika vilindi vya bahari.

31 acHivi ndivyo atawalavyo mataifa,
na kuwapa chakula kwa wingi.

32 adHuujaza mkono wake kwa umeme wa radi,
na kuuagiza kulenga shabaha yake.

33 Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja;
hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.
Au: hutangaza kuja kwake.

Copyright information for SwhKC